Rais wa klabu ya Yanga Eng. Hersi Said ameeleza kuwa mchezo wa fainali wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika msimu huu unaweza kuwakutanisha Al Ahly na Mamelodi Sundowns.
Hersi ameyasema hayo kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Ahly utakaopigwa kwesho nchini Misri majira ya saa moja kamili usiku [19:00] kwa saa za Afrika mashariki.
“Binafsi naamini Fainali ya CAFCL msimu huu itakuwa ni mechi baina ya Al Ahly na Mamelodi Sundowns.”
“Al Ahly ni Moja ya Timu hatari sana Afrika inapofika katika hatua ya mtoano kutokana na uwekezaji wanaoufanya wakifika katika hatua hizo.”
“Mamelodi naipa nafasi kwasababu ni moja ya timu bora kwasasa Afrika, hawa ndio mabingwa wa AFL na sitarajii kama itakuwa ni rahisi kwa wao kuishia Robo au nusu fainali bali na wao pia wana mikakati mizito ya kucheza fainali.”
“Wydad siipi nafasi ya kucheza fainali kwasababu hawapo vyema msimu huu, sidhani kama ni moja ya timu shindani kwasasa Afrika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma”.
- Rais wa Young Africans, Eng. Hersi Ally Said kupitia mahojiano na Televisheni ya Al Ahly.