Nyota wa klabu ya Machester City na timu ya Taifa ya Norway, Erling Haaland amemtaja Leonel Messi kama mchezaji bora zaidi aliyewahi kucheza mpira.
Nafikiri Messi ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kucheza mpira.
Erling Braut Haaland.
Haaland na Messi hawajawahi kucheza pamoja iwe kwenye timu moja au kwenye Ligi moja zaidi wamecheza kwenye mashindano ya Ligi ya mabjngwa Ulaya.
Mshindani mkubwa wa Leonel Messi ni Cristiano Ronaldo na wote kiumri wanaelekea mwisho wa soka lao huku Messi akiwa tayari ametwaa tuzo ya mchezaji bora Duniani nane [8] na Ronaldo akitwaa tano [5].
Haaland na Messi walikutana kwenye usiku wa tuzo za mchezaji bora wa Dunia na Haaland akashuhudia namna Messi anavyoondoka na tuzo yake ya nane ya mchezaji Bora wa Dunia [Ballon d’Or].