Kabla ya mchezo wa Ligi ya mabingwa Barani Ulaya kati ya Napoli na Barcelona hapo jana mmiliki wa klabu ya Napoli aliwekeza zaidi ya €10 Million kwa wachezaji ili tu wafuzu hatua ya robo fainali.
Wachezaji wa klabu ya Napoli wamekosa zaidi ya €10 Million [ TZS Billion 28] ambayo waliahidiwa na mmiliki wa klabu hiyo Aurelio De Laurentiis kama wangefanikiwa kuiondosha Barcelona kwenye hatua ya 16 ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
“Niliweka zaidi ya Million 10.” – Aurelio De Laurentiis akijibu swali kuhusu kuweka ahadi ya pesa kwa wachezaji wa klabu yake kama wataitoa Barcelona.
Napoli ilitoa sare mchezo wa kwanza ikiwa nyumbani [1-1] na jana wakiwa Camp Nou walipoteza kwa goli 3-1 na hivyo klabu hiyo kuondoshwa kwa idadi ya magoli 4-2.
Baada ya kuondolewa kwa Napoli mashabiki wa klabu hiyo kila mmoja amekuwa na maoni yake.
“Ahsanteni kwa kutupeleka kombe la Dunia.”- Giosu.
“Kupoteza mbele ya kikosi cha nne cha Barcelona ni Aibu.” – Gennaro
“Ngoja tuone kwenye kombe la Dunia nini mtafanya lakini mmecheza vibaya.” – Caoscerto.