NBC Premier League

YANGA INAPIGA PASI NYINGI ZAIDI YA SIMBA MSIMU HUU.

Published on

Klabu ya Yanga kwa kipindi cha hivi karibuni imekuwa ikipiga pasi nyingi zaidi chini ya kocha Miguel Gamond kwenye michezo yote wanayocheza kuliko ambavyo wanafanya klabu ya Simba.

Siku zote Simba imekuwa ikipiga pasi nyingi zaidi kwenye mchezo mmoja kuliko Simba lakini kwa kipindi cha hivi karibuni imekuwa tofauti kwa timu hizi mbili.

Yanga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ihefu walipiga zaidi ya pasi 174 kipindi cha kwanza na kipindi cha pili wakapiga zaidi ya pasi 228, wakashinda goli 5-0.

Mchezo wa Simba dhidi ya Singida Fountain Gate, Simba walipigia zaidi ya pasi 189 kipindi cha kwanza, na kipindi cha pili wakapiga zaidi ya pasi 155 wakashinda goli 3-1.

Jumla ya pasi walizopiga Yanga kwenye mechi na Ihefu ni zaidi ya pasi 403, huku Simba dhidi ya Singida FG wakipiga zaidi ya pasi 344.

Kwenye michezo hii miwili Yanga dhidi ya Ihefu na Simba dhidi ya Singida FG, Yanga imepiga pasi nyingi zaidi ya Simba.

Popular Posts

Exit mobile version