CAF Champions League

ARAFAT: SIMBA NA YANGA ZINANAFASI YA KUFUZU NUSU FAINALI.

Published on

Makamu wa Rais wa Yanga SC , Arafat Haji kupitia ukurasa wake wa Twitter amezipa nafasi ya kufuzu kwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika timu za Simba na Yanga.

“Kuhusu nafasi ya Yanga kuvuka hatua ya robo fainali, nafasi kwanza ipo kubwa kwa wote wawili kufika nusu fainali ila kwasasa inahitajika mipango ya muda mfupi ndani ya Mipango ya muda mrefu.

Nyuma ya RS Berkane kutwaa shirikisho, USMA kubeba Shirikisho kulikuwa na mipango inayobadilika kulingana na hatua, natolea mfano timu ambazo hazikuwahi kupewa nafasi kubwa Afrika ila wamefanya vyema hivi karibuni”

“Ukitazama kwa haraka ni sapoti ya serikali na Wadau, inapokuja suala la klabu zao kimataifa wote wanaimba wimbo mmoja kwa maslahi ya kiwanda chao, sehemu ya kwanza ni umoja.” – Arafat Haji, Makamu wa Rais Yanga.

Yanga itakutana na klabu ya Mamelodi Sundowns mwishoni mwa mwezi huu na Simba itakutana na Al Ahly kwenye hatua ya robo fainali na timu zote zikianzia nyumbani kwenye michezo ya kwanza.

Popular Posts

Exit mobile version