Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amewataka Watanzania kutojihusisha kwa namna yoyote ile na timu pinzani zinapokuja kucheza nchini kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika.
Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo kuelekea michezo ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika ambapo Simba itakutana na Al Ahly na Yanga itakutana na Mamelodi Sundowns.
“Watanzania niwaombe sana najua kuna utani wa jadi, lakini kwenye mechi hizi za robo fainali ni mechi za kufa na kupona, hatutegemei kuona Mtanzania yeyote akienda kupokea wageni uwanja wa ndege, ama kuvaa jezi za timu za wageni.”
“Sisi kama Serikali hatutawaachia hili TFF wala Simba na Yanga, kwa hiyo tutahangaika na mtu ambaye tutaona ni msaliti. Tunaomba Watanzania watuelewe na watusamehe kwa sababu tunataka timu hizi zifanikiwe.”
“Kwa hiyo wewe Mtanzania ambaye utaweka kimbelembele kwenda kupokea wageni uwanjani wa ndege, kuwasapoti kwa namna yeyote, hatutakuelewa na tutadili na wewe kwa vile ambavyo tunaona inafaa.”
- Damas Ndumbalo, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Tanzania.
Simba na Yanga zote kwa pamoja zitaanzia nyumbani kwenye michezo yake ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika na kumalizia ugenini.