CAF Champions League

KAMWE: WACHEZAJI 6 HADI 7 WA YANGA WANAANZA MAMELODI SUNDOWNS.

Published on

Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kuwa waandishi wanaidharau sana Yanga lakini wachezaji saba hadi nane wa kikosi cha Yanga wanaweza kupata namba Mamelodi Sundowns.

Hii ina maanisha kuwa Yanga wanaipa nafasi ndogo ya kufuzu ilihali wana kikosi chenye ubora mkubwa pengine kuizidi hata Mamelodi Sundowns yenyewe ambayo wanaipa nafasi ya kufanya vizuri.

“Najua wachambuzi wengi na waandishi hawaipi nafasi Young Africans SC dhidi ya Mamelodi. Nina uhakika Wachezaji sita mpaka saba wanaweza kuanza kwenye kikosi cha Mamelodi. Tunaichukulia poa Young Africans SC kwa sababu tu inatokea Tanzania. Lakini hii Klabu ingekuwa ipo DR Congo ingesifiwa sana kuliko inavyosifiwa sasa.

Mwananchi usisikilize uchambuzi wa mchambuzi yoyote yule. Tusipotezwe kwenye dira yetu. Young Africans SC ikiamua jambo lake hatuwezi kufeli. Nina uhakika kwa zaidi ya asilimia 100 kuwa tunakwenda kushinda mchezo ujao. Mtu akikwambia Mamelodi ina wachezaji wazuri mwambie hata sisi tuna wachezaji bora kuliko wao” – Ali Kamwe.

Kwa upande mwingine Ali Kamwe ametaja kiingilio cha mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns huku akitata mzunguko itakuwa bure na akaainisha sababu za kuweka kiingilie bei ya chini.

“Wote tunakubaliana mechi ya Mamelodi ni mechi kubwa zaidi kwenye robo fainali ya CAFCL msimu huu na Viingilio ni kama vifuatavyo:
??? ? ??,???
??? ? ??,???
??? ? ??,???

Tunafahamu mechi itaisha usiku sana, kwa kuwajali mashabiki wetu na dhamira ya nchi yetu hasa kwenye sekta ya michezo Viongozi wetu wameamua jukwaa la ???????? litakuwa ????”. – Ali Kamwe.

“Viongozi wa Klabu yetu hawana tamaa ya fedha, ndio maana tumepunguza na kuondoa tiketi ya mzunguko kwa lengo la kuhakikisha wengi waje Uwanjani.”

“Tumeweka maslahi ya mpira wa Tanzania mbele. Mechi ya Mamelodi ni kubwa mno lakini kwa kuwa lengo sio fedha ni hamasa basi tunawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi.”

” Kiasi cha fedha ambacho ungelipia tiketi ya mzunguko basi utatumia kama nauli ya usafiri wa kukufikisha uwanjani na baada ya mchezo wetu uweze kurudi nyumbani salama” Aliongeza Ali Kamwe.

Ali Kamwe alieleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umekubaliana kuweka mikakati ya kuwapeleka mashabiki Afrika Kusini.

“Uongozi wa Klabu umekubaliana kuweka mkakati wa kupeleka mashabiki Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano. Kama tulivyofanya wakati wa mchezo wetu wa nusu fainali CAFCC dhidi ya Marumo, ???????? ??? ?????? (kwao kama kwetu) season 2 inaanza na Bei ya kushiriki ni ile ile tshs 2000 tu.”

“Vile vile tumeaanda usafiri wa kwenda Afrika Kusini kwa njia ya basi, ambapo utahitaji kuwa na kiasi cha Tsh 600,000 gharama za kwenda na kurudi. Watu 10 kutoka Morogoro tayari wameshalipa”. Alimaliza Ali Kamwe.

Mamelodi Sundowns wanatarajiwa kuingia nchini Alhamis March 28 kwaajili ya mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa Jumamosi ya March 30 majira ya saa tatu [21:00] usiku.

Popular Posts

Exit mobile version