Nyota wa zamani wa timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Mamadou Gaye ametoa angalizo kwa timu yake hiyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Young Africans siku ya tarehe 30/03/2024.
Sio kwa Yanga tu kwao ni nchi nzima ya Tanzania inausubiri huo mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Tukiongea uhalisia Yanga ni timu kubwa, mwaka 2022 walicheza na timu kutoka Sudan pale Kigali, walisafiri na mashabiki wao kwa gari takribani masaa 20.
Kama Yanga wakishinda mchezo wa kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika, usishangae kuona wamesafiri mashabiki wengi zaidi kuja hapa Afrika Kusini kuiunga mkono timu yao.
Msimu uliopita Yanga waliishangaza Afrika kwa kufika fainali ya kombe la shirikisho, ikawa timu ya kwanza kutoka Tanzania kufika hiyo hatua, kwa imani hiyo inawezekana wanajiuliza kwanini msimu huu tusifike nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika?
Mamelodi Sundowns wakipoteza huu mchezo itawaathiri sana wanachotakiwa kukifanya ni kutafuta matokeo kwenye mchezo wao huu wa kwanza kabla ya marejeano.
Mchezo utakuwa sawa kwa timu zote mbili, tofauti itakuwa kwenye idadi ya wachezaji walio kwenye mfungo, Yanga wana wachezaji wazuri akiwemo Pacome Zouzoua.
Hata wanavyosema baadhi wameumia hiyo ni danganya toto tu “Mind game”, walisema Zouzoua ameumia lakini utashangaa akaitwa kwenye timu ya Taifa.
Mamadou Gaye, nyota wa zamani wa Mamelodi Sundowns akizungumza na Mamelodi Sundowns Podacast.