Klabu ya Al Ahly tayari imetua nchini kwaajili ya mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya klabu ya Simba.
Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Al Ahly kuja kucheza nchini mara mbili kwenye msimu mmoja wa mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika.
Mara ya kwanza walicheza na Yanga kwenye hatua ya makundi na mara hii watakutana na Simba huku mchezo wa Simba na Al Ahly itapigwa saa tatu [21:00] usiku wa Ijumaa.