Nyota wa klabu ya Yanga raia wa Afrika Kusini Skudu Makudubela ameeleza kuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns wataanzia pale walipoishia kwenye mchezo uliopita.
Skudu ameeleza kuwa kuelekea kwenye mchezo huo Yanga itaingia kama Underdog mbele ya Mamelodi Sundowns ambayo imeonyesha mbawa zake na ukubwa wake Barani Afrika kwasasa.
“Nafikiri tutazungumzia ubora wa kikosi ambao Yanga wanao.”
“Kila yanapotokea mapumziko yaliyo kwenye kalenda ya FIFA wachezaji 11 hadi 13 wanaenda kuyatumikia mataifa yao kwenye michezo ya kimataifa.”
“Tuna Diarra ambaye ni miongoni mwa magolikipa bora Afrika, tukimzungumzia Khalid Aucho anaiongoza timu yake ya Taifa, tunaweza kuongea pia kuhusu uzoefu na ubora ambao tunao kwenye timu yetu kutoka mataifa mbalimbali.”
“Tunalipongeza benchi la ufundi wanafanya kazi nzuri sana na wachezaji hawa wazuri ambao wapo kwenye timu.”
“Bila kuwavunjia heshima Mamelodi Sundowns, klabu kubwa Afrika, historia yao inaongea zaidi lakini kama kocha alivyosema tumekuja kama “Underdog” kuonyesha kile ambacho tutaweza.”
“Tunachoweza kuahidi ni kujituma, kama kile tulichokionyesha Dar Es Salaam hakuna cha zaidi wala cha kupungua.”
- Skudu Makudubela, nyota wa klabu ya Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Mchezo wa awali uliopigwa Dar Es Salaam ulimalizika kwa suluhu 0-0, mchezo huu ni muhimu zaidi kwa timu zote mbili kupata matokeo.