Makala Nyingine

YANGA YAIANDIKIA BARUA CAF

Published on

Klabu ya Soka ya Young Africans kupitia kwa Mwanasheria wake, Wakili Simon Patrick wameliandikia barua Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF kuomba uchunguzi kufanyika kwa kile kinachoelezwa kuwepo na viashiri vya upendeleo na upangaji wa matokeo.

Kwenye barua hiyo, Young Africans wanaonekana kutoa shutuma zao kwa Muamuzi kutoka Mauritania Dehane Bedia kukataa bao la Azizi Ki la dakika ya 58 wakiamini kuwa mpira ulikuwa umevuka mstari wa goli lakini yeye hakuenda kujidhirisha kwa ushauri wa VAR hali ya kuwa alienda kujidhirisha tukio la aidha Kadi nyekundu ya moja kwa moja au la lililomuhusisha Lomalisa Mutambala dhidi ya Khuliso Mudau.

Young Africans wanalalamikia kutoridhishwa na uamuzi huo wanaoamini una viashiria vya upendeleo na upangaji matokeo na hivyo kuomba uchunguzi ufanyike na kama itabainika basi sheria ifuate mkondo wake kwa mujibu Kanuni namba XVI kifungu kidogo namba 3.

Popular Posts

Exit mobile version