Mlinda lango wa klabu ya Arsenal David Raya ameandika rekodi mpya ya kuwa golikipa wa kwanza raia wa Hispania kutunza hati safi [Cleansheet] tano mfululizo EPL.
Raya mara ya mwisho amefungwa mwezi January na Taiwo Awoniyi kwenye mchezo ambao Arsenal ilishinda goli 2-1 dhidi ya Nottingham Forest.
Raya amepata Cleansheet dhidi ya Westham, Sheffield United, Burnley, Manchester City na Brighton kwenye dimba la Amex.
Arsenal jana waliichakaza Brighton kwa magoli 3-0 na kuwafanya wajikite kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu nchini England wakifikisha alama 71 walizokusanya kwenye michezo 31.