Nyota wa klabu ya Yanga Stephene Aziz Ki ameeleza kuwa kocha mkuu wa kikosi cha Mamelodi Sundowns alimshauri aongeze uharaka eneo la mwisho tofauti na alivyo sasa kuna muda anachelewa kufanya maamuzi.
“ Kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena aliniambia wewe ni mchezaji mkubwa na una kila sifa, una nguvu na una umiliki mzuri wa mpira miguuni mwako.”
“Rhulani akanishauri niongeze uharaka eneo la ushambuliaji ili kuwa bora zaidi, amenisisitiza kufanya hivyo akiamini kuwa pia naweza na nitakuwa bora zaidi kwa kuwa na namba nzuri ya ufungaji na hili nitalifanyia kazi”