Mwamuzi wa zamani wa FIFA raia wa Afrika kusini Victor Hlungwani ameeleza kuwa mpira uliopigwa na Aziz Ki ukagonga mwamba na kudundia ndani ya mstari wa goli halikuwa goli kama ambavyo VAR iliamua.
Mwamuzi huyo amesifu maamuzi yaliyofanywa na waamuzi kutoka chumba cha VAR ya kulikataa goli lile tofauti na vile ambavyo wengi wanafikiri kuwa lilipaswa kukubaliwa.
“Hatuwezi kusema lile ni goli, Tanzania ule mpira haukuvuka mstari, pingeni muwezavyo lakini CAF hawawezi kukubali, yale ni maamuzi mazuri yaliyofanywa na VAR.”
- Victor Hlungwani, Mwamuzi wa FIFA wa zamani.