Makala Nyingine

KIZAZI CHA MAGOLIKIPA WA KISASA

Published on

Kwa kipindi cha hivi karibuni Ulimwengu wa soka umebadilika sana, umekuwa hauwapi nafasi sana magolikipa ambao hawawezi kuuchezea mpira miguuni.

Nyota wa zamani wa Ajax, Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi, Johan Cruyff yeye aliweka wazi tangu zamani golikipa anayemtaka ni yule anayeweza kuanzisha mashambulizi.

Johan akataja sifa za mshambuliaji anayemtaka kuwa ni yule anayerejea kuisaidia timu pindi inapozidiwa si yule anayesimama mbele muda wote.

“Kwenye timu yangu, golikipa ndiye mshambuliaji wa kwanza na mshambuliaji ndiye mlinzi wa kwanza.”

  • Johan Cruyff, Nyota wa zamani wa Ajax, Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi.

Kwenye Ligi yetu ya Tanzania kwa kipindi cha hivi karibuni timu zetu zimekuwa na huo utaratibu pia wa kusajili walinda lango wenye uwezo wa kuuchezea mpira.

Yanga [Diarra, Mshery], Simba [Ayoub, Ally Salim], Azam [Mustafa], na klabu zingine za Ligi, kwa upande wa washambuliaji pia vivyo hivyo.

Hii ni ishara ya Ligi kukua na pengine kwa miaka ya mbeleni huko inaweza kutawala Afrika kama ilivyokuwa Congo DR miaka ya nyuma.

Popular Posts

Exit mobile version