International Football

JAMAL MUSIALA, LEROY SANE WANAHITAJIKA ANFIELD

Published on

Jamal Musiala na Leroy Sane wako kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na klabu ya Liverpool ili kwenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho ambacho kinanolewa na kocha Mjerumani Jurgen Klopp.

Jamal Musiala amekuwa mmoja wa wachezaji ambao wameanza kuliteka soko la usajili kwa kasi kwani Real Madrid pia wanadaiwa kutaka kumchukua ili akacheze pamoja na kiungo mshambuliaji Muingereza, Jude Bellingham kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Bayern Munich iko tayari kumpa Musiala nyongeza ya mshahara wake wa sasa wa Euro milioni 8 kwa mwaka, jambo ambalo litamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi klabuni hapo. Hata hivyo, kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 anataka kupata timu ambayo itamuhakikishia kupata muda zaidi wa kucheza, hasa kutokana na ukweli kwamba kiwango chake cha uchezaji kimekuwa kikiimarika siku hadi siku.

Popular Posts

Exit mobile version