EPL

FAGIOLI KIFUNGO MIEZI 7, ATOA TAMKO. TONALI, ZANIOLO KUSIKILIZWA KESI YA KUBETI.

Published on

Kiungo wa kimataifa wa Italia na timu ya Juventus ya jijini Turin, Italia, Nicolo Fagioli,22 amefungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi kisischopungua miezi 7 baada ya kukikri na kujisalimisha kuwa alikuwa akijihusisha na “kamari” mbele ya shirikisho la soka la nchini Italia FIGC.

Fagioli, alikri wazi kuwa alikuwa akibashiri kwenye michezo jambo lisilokubalika kwa wanasoka kufanya huku yeye mwenyewe akikiri kuwa kamari kwake imekuwa kama kilevi na mara kadhaa amejitahidi kutafuta washauri na watu wa kummsaidia aweze kuachana na jambo hilo. Sambamba na hukumu hiyo, amekubali pia kuingia kwenye kipindi maalumu cha ushauri.

Aidha hakusita kuonyesha masikitiko yake baada ya hukumu hiyo

Nilidhani ningeanza na kuomba radhi sio tu kwa mashabiki wa Juventus bali jamii nzima ya wanamichezo duniani kwa kosa langu la kijinga, lakini badala yake inanilazimu na kuanza kuonyesha masikitiko yangu makubwa juu ya maneno mabaya dhidi yangu ili nionekane mimi mtu mbaya sana.

Nitatoa tamko langu kuu hivi karibuni.

Katika upande mwengine, wachezaji wengine wahanga wa kashfa hii ni Sandro Tonali wa Newcastle United Nicolo Zaniolo wa Aston Villa ambao wote waliondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kutokana na kashfa hizo kupisha uchunguzi ambao na wao wanatarajiwa kufuata njia hizo hizo alizotumia Fagioli na kusubiri hukumu.

Kwa upande wa Tonali yeye anatarajiwa kupewa hukumu ya si chini ya miezi 12 baada ya yeye pia kukiri kujihusisha na kamari tangu akiwa AC Milan na kuna baadhi ya mechi za Milan “alizibetia”, huku Zaniolo yeye anatarajiwa kutoa maelezo yake mbele ya uongozi wa klabu yake ya Aston Villa kabla ya hatua zaidi huku yeye kesi yake ikiwa tofauti na wenzake.

Zaniolo hajawahi kujihusisha na na kubashiri michezo, kwa mujibu wa wanasheria wake japo alikiri kuicheza Poker na michezo mingine lakini hakujua kwamba hairuhusiwi. Ikibainika ni kweli basi yeye atashushiwa tu rungu la faini.

Mara nyingi kesi za aina hii zina adhabu ya kifungo si chini ya miaka mitatu, lakini kujisalimisha na kukiri wakati mwingine hupunguza ukali wa dhabu hii.

Popular Posts

Exit mobile version