Rais wa shirikisho la soka Duniani (FIFA) Gianni Infatino tayari amewasili nchini Tanzania kwaajili ya ya kushuhudia sherehe za ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League, inayofanyika katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar Es Salaam leo Ijumaa.
Sherehe hizo zitaambatana na mchezo mkubwa unaotarajiwa kutazamwa Dunia nzima kati ya mwenyeji Simba na klabu ya Al Ahly kutoka nchini Misri. Viongozi mbalimbali na wageni mbalimbali tayari wamewasili nchini kwaajili ya kushuhudia ufunguzi huo.
Hii si mara ya kwanza kwa Rais wa shirikisho la soka Duniani FIFA kufika nchini Tanzania, kwani aliwahi kufika hapa kwaajili ya mkutano wa FIFA ( FIFA executive Sumitt 2018), na Agosti 10, 2022 kwaajili ya mkutano wa kawaida wa 44 wa shirikisho la soka Barani Afrika CAF.
Mchezo wa Simba na Al Ahly utapigwa saa 12:00 Jioni katika Dimba la Benjamin Mkapa, mchezo huo utatanguliwa na burudani kadhaa ikiwemo burudani ya msanii mkongwe na nguli Tanzania Mfalme Ally Salehe Kiba.