International Football

RAIS WA FIFA AIPONGEZA TANZANIA.

Rais wa FIFA ameipongeza Tanzania kwa namna inavyopiga hatua katika ukuaji wa soka.

Published on

Rais wa shirikisho la soka Duniani Gianni Infatino kupitia ukurasa wake wa Instagram ameonyesha furaha yake kuwepo nchini Tanzania katika ufunguzi wa michuano mikubwa ya African Football League. Ufunguzi huu utashuhudia mchezo mkali kati ya Simba dhidi ya Al Ahly.

Aidha pia Infatino amemshukuru Rais wa Shirikisho la soka Tanzania Wallace Karia kwa ukaribisho wake mzuri na namna ambavyo wamejadili maendeleo ya soka nchini Tanzania, Pia Infatino amemshukuru Rais wa shirikisho la soka BArani Africa Patrice Motsepe kwa kuweza kuanzisha jambo litakaloendeleza mpira wa Africa.

Nimefurahi kuwa hapa Dar Es Salaam kwaajili ya uzinduzi wa michuano mipya ya African Football League. Pia ninajadili maendeleo ya soka na Rais wa shirikisho la soka Tanzania, Wallace Karia, ambaye ametukaribisha vizuri sana hapa na Marais wa mashirikisho mengine.

Namshukuru pia Rais wa shirikisho la soka Afrika CAF, Patrice Motsepe, and soka zima la Afrika kwa kuanzisha maendeleo ya soka Barani Afrika.

Awali nilikuja hapa Tanzania mwezi Agosti mwaka huu, kila mtu anaona ukuaji na maendeleo ya soka hapa, ni mfano wa matokeo chanya kupitia programu za FIFA kwenda kwa mashirikisho wanachama wetu.

Shukrani zangu ziende kwa kila mmoja ambaye anajihusisha na mpira wa miguu kwenye hii nchi nzuri, lakini pia Afrika nzima, kwa kusambaza furaha kwa vijana wetu wa kiume na wa kike wa hatua zote.

Kwasasa nasubiri kutazama mchezo wa Ufunguzi wa michuano ya African Football League, ni mwanzo wa zama mpya za kuongeza wigo zaidi wa kufuatiliwa, kupelekea ukuaji na maendeleo ya soka la Afrika.

Rais wa FIFA Gianni Infatino ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Popular Posts

Exit mobile version