Mshambuliaji wa klabu ya West Ham United Michail Antonio anaamini kuwa Leonel Messi hastahili kubeba tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mwaka huu licha ya kuisaidia timu yake ya Taifa ya Argentina kubeba ubingwa wa kombe la Dunia, Antonio anaamini kama Messi atabeba mbele ya Haaland itakuwa ni kashfa kubwa.
Mshambuliaji huyo wa Westham United anaamini kuwa Erling Braut Haaland anastahili kubeba tuzo hiyo kutokana na kiwango alichokionyesha msimu uliopita ambapo alifunga jumla ya magoli 52 akiwa na Manchester City katika mshindano yote.
Ninaelewa ni mafanikiwa makubwa kwa Messi kubeba kombe la Dunia, lakini huwezi ukaacha kuiangalia timu iliyobeba mataji matatu na ambacho Haaland amekifanya, amevunja rekodi. Anastahili hiyo Ballon D’or. Kama hataipata basi itakuwa ni kashfa.
Michail Antonio, Mshambuliaji wa Westham United.
Mshambuliaji wa klabu ya Newcastle Callum Wilson nae ameeleza kuwa Ballon D’or inastahili kwenda kwa Erling Haaland kutokana na kiwango alichokionyesha nyota huyo msimu uliopita kwenye klabu yake kama ukiondoa mafanikio ya timu za Taifa.
Aalichokifanya Haaland msimu uliopita hauwezi kukibeza. Kama ukiondoa michuano ya kimataifa na ukalinganisha takwimu zao….. Haaland anastahili kushinda Ballon D’or. Hauwezi ukaangalia kubeba ubingwa wa kombe la Dunia kwa mara ya kwanza ndio ikawa kigezo cha Messi kumpatia tuzo bali kile anachokionyesha kwenye klabu, Messi anacheza Amerika kitu ambacho ni tofauti na Haaland anayecheza Ligi kuu kandanda nchini England.
Callum Wilson, Mshambuliaji wa Newcastle United.
Taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa Leonel Messi huenda akabeba tuzo yake nyingine ya Ballon d’or mwaka huu.