EPL

ANTONIO: TUPENI PESA, BOWEN ATUE ANFIELD.

Published on

Jarrod Bowen amemsifu Mohamed Salah kama mmoja wa wamaliziaji bora wa Ligi Kuu ya chini Uingereza (EPL)- siku chache baada ya kupendekezwa kuchukua nafasi ya mchezaji huyo wa Liverpool na mchezaji mwenzake.

Bowen, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa mmoja wa washambuliaji mahiri zaidi tangu ajiunge na klabu ya West Ham Unied mwaka 2020 na amekuwa akihusishwa mara kwa mara na vilabu katika nne bora. Hata hivyo, uvumi unaomhusisha na kuhamia Anfield umeshika kasi katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, hasa kutokana na kutokuwa na uhakika juu ya mustakabali wa Mohammed Salah. Sawa na Salah, Bowen amekuwa katika kiwango cha hali ya juu msimu huu, akifunga mabao sita katika mechi 11 alizocheza.

Na sasa ameeleza jinsi anavyotamani kuiga uwezo wa fowadi huyo wa Liverpool kuwa katika sehemu sahihi kwa wakati huo. Akizungumza na TNT Sports kabla ya West Ham kupoteza mchezo wa Ligi ya Europa dhidi ya Olympiacos.

Siku zote nilitaka kufunga mabao na kuingia kwenye nafasi ambazo mpira unaweza kukuangukia. Kawaida mimi huwa napenda kuwa ndani ya boksi la timu pinzani ambapo ninajua kuwa nafasi inaweza kuniangukia. Ni kitu ambacho nimekuwa nikifanyia kazi, kwa kweli na baba yangu; anazungumza nami kuhusu hilo, alikuwa mshambuliaji wa kati na anaelewa hilo.

Alisema mchezaji wa West Ham United Jarrod Bowen

Huwa tuna mazungumzo machache tu kuhusu mikimbio tofauti ya kufanya na mahali pa kuwa kwenye boksi la timu pinzani, nadhani Salah ndiye bora zaidi kwake na ni wazi Haaland, pia. Siku zote wanajiweka mahali ambapo wanafikiria watafunga bao. Watu wanasema ni kufunga kutoka yadi nne nje lakini kuna sanaa maalum yake ya kuchukua nafasi hiyo kwenye eneo la hatari na aina ya kutarajia mpira utakapokuwa. Kwa hakika kitu ambacho huwa sikifanyii kazi kwenye uwanja wa mazoezi, labda zaidi kutazama video pekee.

Alisisitiza Jarrod Bowen.

Kauli ya Bowen imekuja siku chache baada ya kutajwa kuwa ndiye mshambuliaji kamili anayefaa kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Mohammed Salah, ambaye anatarajiwa kuwindwa zaidi na vilabu kutoka nchini Saudi Arabia kufuatia ofa zilizogonga mwamba katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Kwa kushangaza, hata hivyo, pendekezo hilo lilitoka kwa Michail Antonio: mmoja wa wachezaji wenzake wa Bowen huko West Ham United.

Kila kitu anachogusa kinageuka kuwa dhahabu sasa hivi. Lakini, itagharimu pesa nyingi, mtu amesaini mkataba wa miaka saba, pesa unazopata kutoka kwa Salah, itabidi utupe! Ana ubora, mguu wa kushoto na anacheza upande wa kulia kama Mo Salah, hivyo ndiye mbadala mzuri, lakini jamani, haitakuwa rahisi kumtoa hapa. Haitakuwa rahisi kwa sababu, Bowen ana mkataba wa miaka saba na klabu yetu ya West Ham United.

Michail Antonio akizungumza kuhusu uwezekano wa Bowen kujiunga na klabu ya Liverpool.

Popular Posts

Exit mobile version