Rais wa heshima wa klabu ya Simba Mohammed Dewji kwa kushirikiana na mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu leo wametangaza wamewateua wajumbe wa Baraza la ushauri la klabu ya Simba,kupitia ukurasa wa Instagram Mohammed Dewji amesema kazi yake kama Rais wa heshima ni kuhakikisha uongozi bora.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu tuanze safari ya Mabadililko Klabu yetu imepiga hatua kubwa sana katika nyanja mbali mbali. Pamoja na maendeleo ambayo Klabu yetu imepiga katika kipindi hiki cha miaka mitano lakini malengo yetu bado hatujayafikia.
Mojawapo ya majukumu yangu kama Raisi wa heshima wa Simba ni kuhakikisha Uongozi na Utawala bora unazidi kuboreshwa kila wakati ili kuzidi kusukuma gurudumu la maendeleo ya Klabu yetu.
Mohammed Dewji kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Walioteuliwa kwenye Baraza hilo ni
- Jaji Thomas Mihayo M/kiti
- Hassan Dalali-Mjumbe
- Ismail Aden Rage-Mjumbe
- Evans Aveva-Mjumbe
- Faroukh Baghoza
- Swedi Nkwabi-Mjumbe
- Azim Dewji-Mjumbe
- Kassim Dewji-Mjumbe
- Musleh Al-Ruweh-Mjumbe
- Mohamed Nassor-Mjumbe
- Mulamu Ng’ambi-Mjumbe
- Octavian Mshiu-Mjumbe
- Prof Janabi-Mjumbe
- Hassan Kipusi-Mjumbe
- Geofrey Nyange-Mjumbe
- Gerald Yambi-Mjumbe
- Moses Kaluwa-Mjumbe
18.Crescentius Magori-Mjumbe
- Juma Pinto- Mjumbe
- Mwina Kaduguda-Mjumbe
- Idd Kajuna-Mjumbe
Sekretariat ya Simba itaratibu mikutano ya Baraza hili la Ushauri. Kazi kubwa ya Baraza hili itakuwa ni kuishauri Bodi juu ya maendeleo ya Klabu yetu ya Simba, Uongozi na Utawala bora.
Mo Dewji aliongeza.