Mchezaji wa zamani wa klabu ya Mancheester United Roy Keane anaamini Bruno Fernandes hana sifa ya kuwa nahodha wa Manchester United licha ya kuwa na kipaji kikubwa. Bruno alipewa kitambaa cha unahodha msimu huu na kocha mkuu wa Manchester United Erik Ten Hag baada ya kumvua nahodha wa awali Harry Maguire.
Bruno hakuonekana kuwatia moyo wenzake na kuwaongezea ari ya kupambana katika mchezo wa jana dhidi ya majirani zao Manchester City, magoli ya Eling Haaland na Phil Foden yalifanya Manchester City ibebe alama zote tatu (3) katika dimba la Old Trafford.
Uongozi wa Bruno Fernandes umekuwa ukitiliwa mashaka na baadhi ya wachambuzi kama Roy Keane, Gary Neville na Micah Richards wote wakikosoa namna ambavyo anaonekana hasa baada ya timu yake kupoteza na namna anavyowahamasisha wachezaji wenzake uwanjani.
Nyota wa zamani wa Manchester United, Roy Keane anaamini ni wakati sahihi kwa Erik Ten Hag kumnyang’anya kitambaa cha unahodha Bruno na kumpatia mchezaji mwingine.
Kitu cha kwanza ambacho ningefanya, ningekuambia umtazame tena, ningemnyang’anya unahodha kabisa kwa asilimia 100. Najua ni maamuzi magumu na ndiyo yaliyo muondoa Maguire kuwa nahodha.
Fernandes hana sifa ya kuwa nahodha, nafikiri ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, sina shaka na hilo, ….. amekuwa akilalamika na kutupa mikono hewani tu muda wote hii haikubaliki. Ningemuondoa kuwa nahodha, ningeanza na hilo kwasababu meneja anaweza kufanya hivyo, haendani na aina ya nahodha ninayemtaka.
Roy Keane akizungumza kupitia Skysport baada ya mchezo wa Manchester United na Manchester City jana.
Manchester United itashuka dimbani tena Jumatano hii kuikabili Newcastle United katika mchezo wa Carabao Cup.