Top Story

AITANA NA MESSI WATWAA BALLON D’OR.

Nyota wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Aitana Bonmati na nyota wa timu ya Taifa ya Argentina Leonel Messi wametwaa tuzo ya mchezaji Bora Duniani.

Published on

Nyota wa timu ya Taifa ya Argentina na klabu ya Inter Miami, Leonel Messi ametwaa tuzo ya nane (8) ya mchezaji bora Duniani ( Ballon D’or) zinazotolewa na shirikisho la soka nchini Ufaransa. Messi amewashinda Kylian Mbappe na Erling Haaland. Wakati wa kukabidhiwa tuzo hiyo Messi amewataja Mbappe na Haaland kuwa siku moja watabeba tuzo hiyo.

Erling Haaland na Mbappe siku moja watashinda Ballon d’or. Erling anastahili zaidi pia, ameshinda Ligi kuu, Ligi ya mabingwa na amekuwa mfungaji bora wa kila mashindano. Tuzo hii leo ilistahili kuwa yako pia.

Leonel Messi baada ya kukabidhiwa tuzo.

Zawadi hii imetokana na kile tulichokipata na timu ya Taifa ya Argentina. Hii ni zawadi kwa wachezaji, makocha na watu wote wa Argentina.

Messi Aliongeza.

Hii ni orodha ya wachezaji 10 bora

  1. Leonel Messi (Inter Miami)
  2. Erling Haaland (Man. City)
  3. Kylin Mbappe (PSG)
  4. Kevin De Bruyne Man. City)
  5. Rodri (Man. City)
  6. Vinicius Jr (Real Madrid)
  7. Julian Alvarez (Man. City)
  8. Victor Osimhen (Napoli)
  9. Benardo Silva (Man. City)
  10. Luka Modric (Real Madrid)

Tuzo zingine zilizotolewa katika usiku wa Ballon D’or ni

  1. Jude Bellingham ( Mchezaji Bora kijana U21 – Kopa Trophy).
  2. Vinicius Junior (Tuzo ya Amani – Socrates Award).
  3. Emiliano Martinez (Golikipa Bora – Yashin Trophy)
  4. Erling Haaland ( Mshambuliaji Bora – Muller Trophy)
  5. Manchester City (timu Bora ya mwaka)

Kwa upande wa wanawake tuzo ya Ballon d’or imebebwa na nyota wa timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Aitana Bonmati ambaye alibeba kombe la Dunia akiwa na timu ya Taifa ya Hispania mwaka huu nchini Australia na kubeba pia Ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na Barcelona na katika michuano yote akiibuka kuwa mchezaji bora.

Aitana mwaka 2023 amepata mafanikio yafuatayo:

  • Ameshinda kombe la Dunia.
  • Ameshinda Ligi ya mabingwa Ulaya.
  • Ameshinda Ligi kuu Hispania.
  • Ameshinda kombe la Ligi.
  • Mchezaji bora UCL.
  • Mchezaji bora kombe la Dunia.
  • Mchezaji bora Supercup.

Popular Posts

Exit mobile version