Simba

SIMBA YALAMBA BILLION 1.5 KUTOKA SBL.

Klabu ya Simba imeingia mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Billion 1.5 na kampuni ya Bia ya SBL.

Published on

Klabu ya Simba hii leo imeingia udhamini wa miaka mitatu (3) wenye thamani ya Billion 1.5 na kampuni ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Pilsner Lager. Udhamini huo utakuwa mahsusi kwaajili ya kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini Ofisa mtendaji wa klabu ya Simba Imani Kajula amesema udhamini huu utasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa klabu.

Ni ubia wa nguvu kabisa, ubia wa Simba wawili. Hii ni package ambayo imekuja wakati mwafaka. Serengeti ni mbia mkubwa sana wa mpira wa Tanzania, huu ni mwendelezo wa kusaidia mpira.

Udhamini huu utasaidia uendeshaji wa klabu, gharama za uendeshaji wa vilabu huwa ni kubwa. Upatikanaji wa fedha ni muhimu sana. Tunawashukuru kukubali kuungana nasi kama wadhamini wa Simba.

CEO Imani Kajula, wakati wa utiaji saini.

Meneja masoko wa kampuni ya Serengeti Anitha Rwehumbiza amesema watashiriki matukio yote ya Simba kwa kuanza na Derby ya kariakoo na hata michezo ya nje ya Dar.

Tulikuwa na lengo la kupata mshirika ambaye ana mashabiki wengi, na tulikuwa na furaha tulipopata taarifa kwamba Simba ipo tayari. Ukiacha kwamba Simba na Pilsner zinaendana kwa rangi na Simba pia Nguvu Moja ya Simba ni ya kuunganisha Watanzia wote na kinywaji chao cha Pilsner Lager.

Meneja Masoko wa Bia za Serengeti, Anitha Rwehumbiza.

Mkurugenzi mtendaji wa Serengeti Breweries amesema mkataba huo utakuwa na thamani ya Billion 1.5 kwa miaka mitatu na lengo ni kukuza soka la Tanzania.

Udhamini huu utakuwa na thamani ya Tsh. 1.5 bilioni. Kwa udhamini huu tunaamini utasaidia kukuza michezo nchini kwetu. Simama Imara, Songa Mbele Kama Simba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti ​Breweries Limited, Obinna Anyalebechi.

Popular Posts

Exit mobile version