Nyota wa klabu ya Wydad Casablanca Osama Faloh ameripotiwa kufariki Dunia baada ya kupata majeraha kutokana na ajali ya gari aliyoipata wiki kadhaa zilizopita.
Oussama alikuwa akicheza eneo la Ulinzi, amefariki akiwa na umri wa miaka 24. Kupitia ukurasa wa Instagram klabu ya Wydad AC imetoa taarifa ya kifo cha nyota huyo na kutoa salamu zake za pole kwa ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.
Kwa masikitiko makubwa, uongozi wa klabu ya Wydad Athletic umepokea taarifa za kifo cha mchezaji wetu Osama Faloh na kwa huzuni kubwa Mr. Saeed Al-Nasiri anatoa salamu za pole kwa niaba ya wachezaji, viongozi wa klabu na wafanyakazi wote kwa familia na jamaa wote walioguswa na msiba huu, tunamuombea mwenyezi Mungu ampunguzie adhabu ya kaburi, tumetoka kwake na kwake tutarejea.
Taarifa kutoka kwa Rais wa klabu ya Wydad AC Saeed Al-Nasri.