Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo miwili kupigwa nchini, Mashujaa vs Singida Fountain Gate, Geita Gold vs Tabora United.
Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo miwili kupigwa nchini. Hizi ni takwimu za michezo yote miwili itakayochezwa leo.
16:00 MASHUJAA vs SINGIDA FOUTAIN GATE
UWANJA: Lake Tanganyika, Kigoma.
Timu hizi hazijawahi kukutana kwenye michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara, hii itakuwa mara ya kwanza kwa timu hizi mbili kukutana.
Mashujaa inanolewa na Abdallah Bares ambaye amewahi kuzifundisha klabu kadhaa ndani ya Ligi kuu Tanzania Bara.
Mashujaa wanaingia katika mchezo huu wakiwa na rekodi ya kupoteza mchezo mmoja (1) pekee kwenye uwanja wao wa nyumbani, imeshinda michezo miwili (2), na imetoa sare mchezo mmoja (1), imecheza jumla ya michezo minne (4) ikiwa nyumbani.
Mashujaa iecheza michezo saba (7) kwa ujumla hadi hivi sasa msimu huu, imepoteza michezo mitatu (3), imetoka sare mara mbili (2) na kuibuka na ushindi mara mbili (2), ipo nafasi ya kumi (10) ya msimamo wa Ligi kuu na alama nane (8).
Hadi hivi sasa Mashujaa imefunga magoli manne (4) n imefungwa magoli sita (6).
Singida Fountain Gate imecheza michezo sita (8) ya Ligi msimu huu, imeshinda michezo miwili (2), imepoteza michezo miwili (3), imetoa sare michezo mitatu (3), ipo nafasi ya tisa (9) ya msimamo wa Ligi kuu ikiwa na alama tisa (9).
Singida Fountain Gate imecheza michezo mitatu (3) ikiwa ugenini, imeshinda michezo miwili (2), na imepoteza mchezo mmoja.
Singida imefunga magoli nane (8) na kufungwa magoli kumi (10).
Leo zitakutana timu mbili ambazo zina rekodi bora, Singida ikiwa ugenini inaonekana kuwa bora sana na Mashujaa ikiwa nyumbani inakuwa timu hatari sana.
10:00 GEITA GOLD vs TABORA UNITED
UWANJA: Nyankumbu, Geita.
Timu hizi ni kwa mara ya kwanza zinakutana katika michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara.
Geita Gold ikiwa mwenyeji wa Ligi na Tabora United huu ndio msimu wake wa kwanza tangu apande daraja msimu uliopita.
Geita Gold imecheza michezo nane (8), imeshinda mchezo mmoja (1) pekee, ikitoa sare michezo mitatu (3), na kupoteza michezo minne (4), imefunga magoli matano (5), imefungwa magoli 11, imekusanya alama sita (6) ipo nafasi ya 15.
Geita Gold ikiwa nyumbani imecheza michezo mitatu (3), imetoa sare mchezo mmoja (1) na kupoteza michezo miwili (2), wamefungwa magoli saba (7) wakifunga magoli matatu (3).
Tabora United hadi hivi sasa imecheza michezo nane (8) ya Ligi kuu, ikishinda michezo miwili (2), imepoteza michezo miwili (2), imetoka sare mara nne (4), imefunga magoli matano (5), imefungwa magoli saba (7), ipo nafasi ya nane (8) ya msimamo wa Ligi.
Tabora United imecheza michezo mitano (5) ugenini, haijapata ushindi wa aina yoyote ile, imepoteza michezo miwili (2) na kutoa sare michezo mitatu (3), haijafunga goli lolote ikiwa ugenini msimu huu, imefungwa magoli matano (5).
Hii pia ni miongoni mwa mechi bora za kutazama kwasababu timu zote mbili hazina mazingira rafiki kuelekea katika mchezo wa leo, Tabora United haina matokoe mazuri ugenini na Geita Gold haina matokeo mazuri nyumbani.