Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amewataka wamiliki wa Manchester United kubaki na Erik Ten Hag kama wanahitaji mabadiliko kwenye timu.
Klabu ya Manchester United licha ya kuanza vibaya katika michezo yake ya kwanza ya Ligi kuu nchini England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 61 kupita, bado kocha wa zamani wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson anamwamini Erik Ten Hag kuwa ataibadilisha klabu hiyo na kuwa tishio.
Magazeti nchini England yanaripoti kuwa Ferguson anamtetea sana Erik Ten Hag na kusema kuwa itakuwa ni makosa makubwa kumuondosha Erik kwenye kipindi hiki.
Matokeo mabaya anayoyapata na kile kinachoendelea ndani ya klabu hiyo yanafanya maisha ya Erik Ten Hag ndani ya klabu hiyo yawe mashakani. Lakini bado Sir. Alex yupo pamoja na Mholanzi huyo. Ferguson amewataka wamuamini kwani anauwezo wa kuibadili klabu hiyo na anawaambia wamiliki wa manchester United waendelee kumuaini.
Kwa kujibu wa taarifa zinasema kuwa ushindi wa manchester United dhidi ya Fulham umenusuru kibarua cha Erik Ten Hag lasivyo angeondolewa, kibarua kinachofuata ni Ligi ya mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Copenhagen ambapo anatakiwa kupambana apate matokeo mazuri.