Kadi nyekundu aliyoonyeshwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford imeacha maswali mengi kwa mashabi na wachambuzi huku UEFA pia ikiwa haielewi ilitoka kwa sababu gani
Manchester United jana ilikuwa ikicheza mchezo wake mwingine wa Ligi ya mabingwa Barani Ulaya nchini Denmark dhidi ya Copenhagen katika hatua ya makundi, mchezo ambao ulishuhudia Manchester United ikipokea kipigo cha goli 4-3.
Manchester United ilikuwa ikiongoza magoli 2-0 kabla ya Marcus Rashford kutolewa nje ya uwanja dakika ya 42 kwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga mlinzi wa klabu ya Copenhagen, Elias Jelert eneo la Enka kwenye mguu wake wa kushoto.
Kadi nyekundu ya Rashford imewachanganya wengi ikiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United Paul Scholes aliyelalamika kuwa refa alifanya maamuzi yasiyo sahihi licha ya kutazama VAR.
Shirikisho la soka Barani Ulaya (UEFA) liliendelea kuwachanganya zaidi watu baada ya kutoa maelezo kwenye ukurasa wao kuwa,
Mshambuliaji ametolewa nje kwa kosa la kumshika Jalert na mikono yake
Maelezo ya kadi nyekundu yaliyotolewa na ukurasa wa UEFA.
Hata UEFA wenyewe hawayaelewi yale maamuzi.
Mchambuzi mmoja alisema.
Rashford ametolewa nje kwa kumkanyaga Jalert.
UEFA baadae ilirekebisha Chapisho chapisho hilo.
Mchambuzi wa soka Barani Ulaya Hargreaves ameesema Rashford alikuwa akiulinda mpira na hakuwa na dhamira ya kufanya madhambi.
Nakataa miaka million, Marcus alikuwa anajaribu kuweka mguu mbele ya mpira.
Hargreaves, Mchambuzi wa soka.
Mchezaji wa zamani wa Arsenal ambaye pia ni mchambuzi wa soka aliandika kupitia ukurasa wake wa X kuwa haikustahili kadi nyekundu,
Haiwezekani kuwa ile ilikuwa ni kadi nyekundu kwa Rashford.
Ian Wright.
Hakuna uwezekano wa kuwa ile ni kadi nyekundu, nachukia hizi video zinazoonyesha taratibu na hizi picha ambazo zinaonyesha ubaya wa kitu mara 10.
Jamie Carragher, aliandika kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya kadi nyekundu kutolewakwa Rashford Copenhagen wakasawazisha magoli yote mawili kabla ya mapumziko ubao ukasoma 2-2, magoli mawili ya kipindi cha kwanza ya Manchester United yalifungwa na Easmus ojlund na mawili ya Copenhagen yakifungwa na Mohamed Elyounoussi na Diogo Goncalves.
Penati ya Bruno Fernandes baadae iliwafanya waongoze mchezo kabla ya Luka Lerager kuisawazishia timu yake na baadae Roony Bardghji akaipatia goli la ushindi Copenhagen.
Manchester United sasa ipo mkiani mwa msimamo wa kundi na mchezo unaofuata itakuwa dhidi ya Galatasaray na kama watapoteza wataondolewa rasmi katika mashindano hayo wakiwa na mchezo mmoja mkononi.