Uhamisho

ENG. HERSI: TUTAONGEZA WACHEZAJI JANUARY.

Published on

Rais wa klabu ya Young Africans Eng. Hersi Ally Said amesema kuelekea dirisha dogo la usajili la mwezi January wanatarajia kufanya maingizo ya wachezaji wapya katika maeneo ambayo yanaonekana kuwa na uhitaji kwenye kikosi chao.

Hersi ameeleza kuwa tayari ameshaketi na mwalimu pamoja na bechi la ufundi ili kuainisha nafasi ambazo zinapaswa kufanyiwa maingizo mapya mwezi January, eneo ambalo linatajwa zaidi kuwa linategemewa kuletewa ingizo jipya ni eneo la ushambuliaji pamoja na beki wa kati.

Dirisha dogo wategemee ongezeko la Wachezaji kwa baadhi ya maeneo kwakuwa tayari tumeshakaa na Mwalimu pamoja na benchi lake kutambua maeneo hayo, kifupi kuendana na ratiba ngumu tutarajie usajili wa baadhi ya Wachezaji wapya.

Eng. Hersi Said, Rais wa Klabu ya Young Africans.

Popular Posts

Exit mobile version