Aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Simba Mbrazil Roberto Oliviera amesema anaweza kurejea tena Tanzania wakati wowote ule pindi atakapohitajika lakini pia amewashukuru mashabiki wa Simba waliompa ushirikiano wakati wote aliokuwa Tanzania.
Nimehudumu Tanzania miezi 11, nimepoteza mchezo mmoja pekee tangu nijiunge na Simba, ahsanteni sana mashabiki wa Simba, tuko pamoja. Mashabiki wa Simba ni wazuri wanaisapoti sana timu na wachezaji wao.
Watu waliniamini kila siku, hongera kwao na baadae naweza nikarejea tena Tanzania, naondoka hapa nikiwa na jina jipya la utani la Mr. Objective.
Roberthino, kocha wa zamani wa klabu ya Simba.
Robertinho aliondolewa na klabu ya Simba kama kocha mkuu kufuatia kipigo walichokipita Simba kutoka kwa mpinzani wake wa karibu klabu ya Yanga cha 1-5.