Mastaa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameendelea kuwasili kujiunga na wenzao kambini kujiwinda na michezo ya kalenda ya kimataifa ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, Dhidi ya Morocco na Niger.
Wachezaji wa Taifa Stars wanaocheza Ulaya, Haji Mnoga, Ben Starkie na Golikipa Kwesi Kawawa ni miongoni mwa waliowasili leo.
Mchezaji wa Taifa Stars, Saimon Msuva akiwasili nchini
Taifa Stars itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Morocco tarehe 21/11/2023 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam, Saa 4 usiku.