Kikosi cha wachezaji wa klabu ya soka ya Simba ambao hawapo kwenye timu zao Taifa, kimeanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na michezo ijayo ya kimashindano ikiwemo mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast, utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Jumamosi ya Novemba 25 saa 10.00 Jioni.