Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na nahodha wa timu ya Taifa ya Nigeria John Obi Mikel amesema mwaka 2013 alistahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora Barani Afrika mbele ya Yaya Toure ambaye ndiye alikuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka ule.
Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea anaamini katika uwezo aliouonyesha mwaka huo na mafanikio makubwa aliyoyapata hayakutazamwa kama sifa ya yeye kupata tuzo hiyo mbele ya nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure.
Mwaka huo Mikel alikuwa mhimili mkubwa kwenye timu ya Taifa ya Nigeria iliyoshinda ubingwa wa Afrika (AFCON) na kutajwa kuwa miongoni mwa wachezaji bora. Licha ya mafanikio hayo Obi Mikel alimaliza katika nafasi ya pili kwenye tuzo hizo nyuma ya Yaya Toure.
Mwaka 2013, nilistahili kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika (CAF Award), Nilibeba ubingwa wa mataifa ya Afrika, mwaka wa nyuma yake nilibeba Kombe la Ligi ya mabingwa Barani Ulaya, na Europa League mwaka 2013 na Yaya Toure hakushinda.
Hakushinda chochote na nilifika kwenye sherehe za tuzo, huku nikiamini naenda kubeba ile tuzo, taarifa zilikuwa kwamba naenda kushinda ile tuzo, niliambiwa na CAF naenda kushinda.
Obi Mikel amezungumza.
Obi Mikel ameibua maswali mengi kuhusu uhalali na uwazi wa kuchagua majina yanayoingia kwenye king’anyiro cha kugombea tuzo ya mchezaji bora Barani Afrika.