Uhamisho

KACHWELE AULA VANCOUVER WHITECAPS.

Published on

Nyota mshambuliaji wa timu ya vijana ya Tanzania Cyprian Kachwele ametambulishwa rasmi kwenye kikosi cha klabu ya Vancouver Whitecaps ya nchini Canada. Kachwele amelelewa kwenye timu ya vijana ya Azam FC ambapo amecheza kwa mafanikio makubwa akiwa na kikosi hicho kwenye Ligi ya vijana. Cyprian alijiunga na kikosi hicho mwaka 2020 akitokea Manganja Football Academy.

Klabu hii pia iliwahi kutumikiwa na nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Young Africans Nizar Khalfan ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa na kikosi hicho cha Vancouver Whitecaps.

Hapo jana, Cyprian alipokea mwaliko wa kuhudhuria hafla fupi ya kumkaribisha nchini Canada kutoka Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki [Mataifa yanayozungumza Kiswahili], lengo la hafla hii ni kumjenga kisaikolojia nyota huyo, lakini pia kumsaidia kupata wenyeji na kumuondolea mawazo ya nyumbani anapokuwa huko. Hafla hii hufanyiwa nyota yoyote anayeenda kucheza nchini Canada kutoka Afrika Mashariki.

Kwenye chakula hicho cha jioni alikuwepo pia kocha wa timu za vijana za Vacouver Whitecaps, meneja wa programu za kijami, Meneja wa timu na viongozi wengine, lengo ni kumtambulisha kijana kwenye Jumuiya hiyo.

Hizi hapa takwimu za mshambuliaji kinda Cyprian Kachwele tangu alipojiunga na timu ya vijana ya Azam FC na baadae kupanda timu kubwa kabla ya kupata nafasi ya kwenda nje ya nchi ambapo kwa sasa amesajiliwa na Vancouver Whitecaps FC ya Canada .

Akiwa Azam FC umri chini ya miaka 17 [Under 17] msimu wa 2020/21 alicheza mechi 17 na kufunga magoli 14 .

Msimu uliofuata 2021/22 akiwa bado timu ya vijana alifunga magoli 20 kwenye mechi 17.

Msimu uliofuata alipanda timu ya vijana chini ya miaka 20 [Under 20] 2022/23 alicheza mechi 5 rasmi na kati ya hizo alifunga mabao manne [4].

Mwezi wa nane alipandishwa timu ya wakubwa [Senior Team ] na mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Altar Solar ya Djibouti [ mechi ya kirafiki] mechi kubwa dhidi ya timu yenye mastar kama Alexander Song na Solomon Kalou .

December 9, 2022 alicheza mechi rasmi ya mashindano dhidi ya Malimao FC mechi ya FA Cup hatua ya 16 bora na alifunga mabao mawili [2] na kutoa assist moja.

Baadae alicheza mechi ya ligi kuu [NBC Premier League ] dhidi ya Singida Big Stars, mechi ambayo Azam ilipoteza kwa bao 1-0.

Mshambuliaji huyo pia ametafutiwa mwalimu atakayemfundisha lugha ya kingereza ili iwe rahisi kuwasiliana akiwa huko. Kila lakheri Cyprian Kachwele katika utumishi wako mpya huko Canada, ipeperushe vyema bendera ya Tanzania.

Popular Posts

Exit mobile version