International Football

FIFA KUINGIA MKATABA NA SAUDI ARAMCO.

Published on

Shirikisho la soka Duniani FIFA linatarajiwa kuingia mkataba wa udhamini na kampuni ya mafuta na gesi ya nchini Saudi Arabia (Saudi Aramco). Mkataba ambao utagharimu kiasi cha $ 100 kwa mwaka kwa miaka 10 ijayo.

Kampuni hii ya mafuta na Gesi ilianzishwa May 29, 1933 miaka 90 iliyopita na makao yake makuu yanapatikana Dhahran, Saudi Arabia. Kampuni hii inaongozwa na Amin Nasser ambaye ni Rais na mtendaji mkuu wa kampuni hiyo pamoja na mwenyekiti wake Yassir Al-Rumayyan.

Serikali ya Saudi Arabia ina miliki hisa asilimia 90, na mwaka uliopita [2022] ilitajwa kama kampuni ya pili Duniani iliyokusanya mapato mengi zaidi, ikikusanya mapato ya US $ 535. 188 Billion. hii ndio kampuni kubwa ya usambazaji wa mafuta Duniani.

Popular Posts

Exit mobile version