Top Story

KARUME BOYS YAPATA MWALIKO WA RAIS IKULU.

Published on

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 15 ya Zanzibar ‘Karume Boys’ mara baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Afrika mashariki na kati kwa umri chini ya miaka 15 iliyofanyika nchini Uganda, leo imepata mwaliko kutoka kwa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh. Dkt. Hussein Ali mwinyi kwaajili ya kupata chakula cha pamoja na kuwapongeza nyota hao kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya.

Kikosi hicho pia kimepokea mwaliko kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amepiga simu kuwaalika vijana hao Ikulu ndogo ya Tunguu iliyopo Visiwani Zanzibar kwaajili ya kupata chakula cha pamoja na kuwapongeza kwa kutwaa kombe la CECAFA U15.

Karume Boys walitwaa ubingwa baada ya kuwachapa mabingwa watetezi na wenyeji wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Uganda chini ya miaka 15 kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya goli 1-1 waliyoipata dani ya dakika 90.

Huu ni mara ya kwanza kwa timu ya Taifa ya Zanzibar kurejea na kombe katika michuano ya ngazi zote ambazo timu hizo hupata nafasi ya kushiriki.

Popular Posts

Exit mobile version