CAF Champions League

YANGA YAACHIA JEZI MPYA ZA CAF CL 2023/24.

Published on

Klabu ya Young Africans leo imeachia jezi zake mpya itakazozitumia katika mashindano ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika msimu huu wa 2023/24. Yanga imetambulisha jezi zenye rangi tatu tofauti, Jezi ya Kijani ikiwa ya nyumbani, njano ya ugenini na Blue ni jezi ya tatu.

Yanga itashuka dimbani Ijumaa hii kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ugenini nchini Algeria dhidi ya CR Belouizdad mechi ambayo itachezwa saa nne kamili [22:00] usiku katika uwanja wa Stade du 5 Juillet 1962 uliopo katika Jiji la Algers.

Popular Posts

Exit mobile version