Chelsea bado haijaamua kama Thiago Silva atasalia katika klabu hiyo msimu ujao kwani mkataba wa beki huyo utaisha msimu wa joto.
The Blues watafanya uamuzi kuhusu mustakabali wa Mbrazili huyo mwaka ujao, gazeti la Evening Standard linaripoti. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 yuko tayari kurefusha muda wake wa kukaa Stamford Bridge na anasalia kuwa mtu muhimu chini ya Mauricio Pochettino, akiwa ameanza mechi zote 13 za Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL) hadi sasa msimu huu.
Chelsea hawana uhakika kuhusu kuongeza mkataba wa Silva kwa kuwa wanafikiria kusajili beki wa kati wapya kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Tayari wametumia pesa nyingi kuwanunua makinda kama Wesley Fofana, Benoit Badiashile na Axel Disasi na wanaweza kutafuta kusajili mchezaji mdogo zaidi kwa msimu ujao.
Beki huyo wa kati amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kucheza na timu hiyo ya London kwenye mchezo walipoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle Jumamosi. Alifanya makosa makubwa kwa kumzawadia Joelinton bao lililowawezesha Newcastle United kuongoza kwa mabao 3-1
Napenda kuomba radhi kwa kila mtu kwa kushindwa, hasa kwa wachezaji wenzangu wanaoniamini na kuniunga mkono kila siku. Ninachukua jukumu kamili. Wacha tukusanye nguvu na turudi kwa nguvu zaidi.
Thiago Silva kizungumza baada ya mchezo huo.
Nyota huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain na AC Milan atasubiri klabu yake kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake. Timu yake ya zamani ya Fluminense inasemekana kuwa na hamu ya kumrejesha nchini kwao, lakini kutokana na wanawe wawili wanaocheza kwa sasa katika akademi ya Chelsea, huenda akapendelea kusalia London.