EPL

KOCHA BRIGHTON AKERWA NA WAAMUZI.

Published on

Nahodha wa kikosi cha Brighton, Lewis Dunk amekuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi baada ya kumtolea lugha isiyofaa mwamuzi Anthony Taylor baada ya kutoa penati kwa Nottingham Forest kwenye mchezo wa Ligi kuu uliomalizika kwa Brighton kuibuka na ushindi wa goli 3-2 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hata hivyo Lewis kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu alikuwa ameonyeshwa kadi nyingine ya njano. Mchezaji wa mwisho kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kosa la kujibizana na refa alikuwa ni Alan Smith, January, 2008 wakati Southampton anapoteza goli 6-0 mbele ya Manchester United.

March, 2012 mchezaji wa zamani wa Sunderland Lee Cattermole alipewa kadi nyekundu baada ya kujibizana na mwamuzi kwenye mchezo dhidi ya Newcastle lakini mchezo ulikuwa umemalizika.

Baada ya kadi hiyo De Zerbi akasema asilimia 80 ya waamuzi wa soka England anawachukia sana kutokana na maamuzi yao mabovu wanapokuwa uwanjani.

Nasema ukweli na kwa uwazi, asilimia 80 ya marefa wa England siwapendi.

Sio mambo mapya, siwapendi na sizipendi tabia zao wakiwa uwanjani.

De Zerbi, kocha mkuu wa Brighton.

Kwasasa klabu ya Brighton inakabiliwa na majeruhi wengi sana, jambo ambalo linamfanya De Zerbi ashindwe kutumia mbinu zake zote, na sasa nahodha wake atakosekana kwenye michezo miwili ijayo.

Popular Posts

Exit mobile version