Klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Esperance de Tunis katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Ijumaa hii ya December 1, 2023.
Al Hilal imechagua kuutumia uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania kutokana na hali ya usalama kutokuwa rafiki nchini Sudan.
Al Hilal itatumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika michezo yake yote ya kimataifa msimu huu. Al Hilal ipo kundi C pamoja na klabu za ES Sahel, ES Tunis na Petro Atletico de Luanda.
Al Hilal imepoteza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ikiwa ugenini kwa goli 1-0 dhidi ya Petro Atletico de Luanda ya nchini Angola.
December 1, 2023.
16:00 Al Hilal vs ES Tunis
Uwanja: Benjamin Mkapa