Klabu ya Young Africans inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara imemuongezea mkataba mpya mlinzi wake wa kati Ibrahim Hamad Abdullah utakaomfanya asalie klabuni hapo hadi mwaka 2027.
Yanga ilimuongezea mkataba Ibrahim tangu mwaka jana lakini mambo yalikuwa hayajakaa sawa kati ya Yanga na wamiliki wa mchezaji huyo Kikosi maalumu cha kuzuia magendo Zanzibar [KMKM] lakini baada ya mazungumzo ya pande zote mbili hatimae wametangaza rasmi hii leo.
Kwa mujibu wa taarifa zilikuwa zinadai kuwa Jeshi lilimtaka nyota huyo arejee kazini na asiongeze mkataba mpya lakini Uongozi wa Yanga kupitia kwa Rais Eng. Hersi Said ukafanya jitihada za kuzungumza na uongozi wa Jeshi la KMKM na hatimae wakafikia makubaliano ya Bacca kisalia Yanga.
Ibrahim kwa mujibu wa mkataba mpya analipwa takribani Million 10 kwa mwezi. Yanga ilimsajili Ibrahim kutoka KMKM na kumpatia mkataba wa mwaka mmoja ambao ulikuwa unamfanya alipwe Million 2 kwa mwezi.