Klabu ya Kagera Sugar inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara imefanya semina ya siku mbili kwa viongozi na wachezaji wa klabu hiyo ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika majukumu yao.
Semina hiyo imeanza jana December 28 na itatamatika leo December 29.
Kwasasa Kagera Sugar ipo nafasi ya nane [8] ya msimamo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara ikiwa na alama 13 katika michezo kumi [10] iliyocheza hadi hivi sasa.