CECAFA

KOCHA TANZANIA ALIA NA HALI YA HEWA BAADA YA KIPIGO.

Published on

Timu ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 18 imekubali kichapo hii leo kutoka kwa timu ya Taifa ya Sudan Kusini katika mashindano ya Cecafa U18 yanayoendelea huko nchini Uganda.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwwnza kina tamatika Tanzania U18 ilikuwa inaongoza 1-0 lakini vijana wa Sudan Kusini U18 walirudi imara kutoka mapumziko na kufunga magoli mawili [2] ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili na kufanya dakika 90 zimalizike kwa matokeo ya Tanzania U18 1-2 Sudan Kusini.

Kocha mkuu wa kikosi cha Tanzania U18 amesema chanzo cha timu yake kupoteza ni pamoja na hali ya hewa kutokuwa rafiki kwa upande wao.

Mchezo ulikuwa mgumu sana, hali ya hewa ilituathiri, kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho vijana walikuwa chini sana leo.

Kocha mkuu wa kikosi cha Tanzania U18.

Baada ya kutoka nyuma na kupata ushindi kocha mkuu wa kikosi cha Sudan Kusini chini ya miaka 18 amesema walikuwa wamejipanga zaidi na mchezo huu kwasababu walipoteza mchezo wao wa kwanza.

Tulipoteza mchezo wa kwanza tukarejea kujipanga mazoezini ndio maana leo tumeonyesha kiwango kile na tumepata matokeo.

Kocha mkuu wa Sudan Kusini U18

Tanzania ilipata ushindi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda U18.

Sudan Kusini U18 pia ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zanzibar U18 kwa kupoteza goli 1-0.

Tanzania U18 sasa itasubiri mchezo wake wa mwisho dhidi ya Zanzibar U18 ili kuijua hatma yake ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hii ya Cecafa.

Popular Posts

Exit mobile version