Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Ndg. Gerson Msigwa ametoa maoni yake baada ya kumalizikia kwa mchezo wa ligi ya mabingwa CAF kati ya Yanga na Al Ahly uliokwisha kwa Sare ya 1-1.
Akiongea na Daudasports, Katibu Msigwa alisema kuwa bado safari ni ndefu na mwendo hauridhishi sana kwa timu zote mbili zinazowakilisha nchi yani Simba na Yanga lakini pia hakusita kuzipa nguvu timu hizo kuendelea kupambania taifa na kuwapa moyo mashabiki kuwa nafasi bado ipo.
Daudasports tumekuwekea kwa urefu mazungumzo hayo kwenye chaneli yetu ya youtube.
BADO NAFASI IPO, TIMU ZETU ZIENDELEE KUPAMBANA- MSIGWA
Young Africans wamefikisha alama 1 wakiwa nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Kundi D linaloongozwa na Al Ahly mwenye alama 4 wana kibarua kizito cha kuhakikisha wanashinda walahu mechi 3 zijazo wakianza na mchezo dhidi ya Medeama kwenye mchezo utakaopigwa Ghana, Tarehe 08, Disemba 2023.