NBC Premier League

BARESI: TUNAPITIA KIPINDI KIGUMU.

Published on

Timu ya Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma haijapata ushindi tangu ilipoifunga Ihefu kwenye mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa Septemba 16, jambo ambalo limemfanya kocha wa timu hiyo, Abdallah Mohamed ‘Baresi’ kukiri hali ni ngumu kwao, lakini hawana namna wanajipanga kabla ya kuwakabili majirani zao wa Tabora United kesho mjini Kigoma.

Mashujaa juzi ilikumbana na kichapo cha tano mfululizo katika mechi sita ilizocheza tangu ilipoonja ushindi wa mwisho kwa kuchapwa mabao 3-2 na KMC mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kocha Baresi alisema mambo ni magumu na wapo kwenye hali ngumu, lakini wanaendelea kupambana.

Tulianza vizuri tumeonyesha ushindani wa kutosha sasa tunapitia mambo magumu ambayo ni muda wa kurekebisha kabla ya kurudi tulikotoka tunarudi tumekaribishwa na sasa ni wakati wa kupambana

Bares alikiri kupitia wakati mgumu huku akifunguka kuwa anahitaji kubadilika kimbinu kwani tayari wapinzani wake wamemjua njia zake hivyo wanatumia madhaifu hayo.

Popular Posts

Exit mobile version