NBC Premier League

YANGA KUNG’OA MSHAMBULIAJI CAMEROON.

Published on

Klabu ya Yanga imefanya mazungumzo ya awali na wawakilishi wa mshambuliaji wa Dynamo Doula, Leonel Ateba Mbida (24)ya kuihitaji saini yake dirisha dogo la mwezi January.

Leonel amewahi kucheza kwenye moja ya klabu kubwa nchini Cameroon ya Cotton Sport na PWD Bamenda zinazoshiriki Ligi kuu ya nchini Cameroon.

Leonel tayari ameitumikia timu ya taifa ya Cameroon mchezo mmoja mwaka huu dhidi ya Libya kufuzu kombe la dunia siku chache zilizopita.

Msimu huu ameitumikia klabu yake kwenye michezo miwili [2] na amefunga magoli mawili [2].

Popular Posts

Exit mobile version