CECAFA

TANZANIA YACHAPWA NA KENYA CECAFA U18.

Published on

Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 18 imeondoshwa kwenye mashindano ya CECAFA U18 katika mchezo wa nusu fainali ulipigwa hii leo katika uwanja wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.

Hii ilikuwa ni miongoni mwa nusu fainali bora iliyozikutanisha timu mbili zenye uwezo wa kucheza mpira kwa asilimia kubwa.

Dakika tisini za mchezo huo zilimalizika kwa suluhu (0-0), zikaongezwa dakika zingine 30 na matokeo yakaendelea kusalia hivyo hiyo.

Mchezo huo uliamuliwa kwa mikwaju ya penalty iliyoishuhudia Kenya ikisonga mbele katika hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa goli 4-3.

Kenya U18 sasa itakutana na Uganda katika hatua ya fainali huku Tanzania ikikutana na timu ya Taifa ya Rwanda katika hatua ya kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hii.

Popular Posts

Exit mobile version