Mmiliki wa klabu ya Medeama ya nchini Ghana, Moses Armah “Parker” amezungumza kuwa wanauhakika wataifunga Yanga katika mchezo wa Ijumaa hii wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Parker amesema kuwa watafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii kutoka kwenye hili kundi hili mbele ya CR Belouizdad, Al Ahly na Yanga.
Wachezaji wangu walifanya vizuri mchezo wetu dhidi ya CR Belouizdad, walikuwa na shauku kubwa ya mchezo kabla ambayo ilitusaidia.
Tutacheza dhidi ya Yanga SC Ijumaa na tutashinda tena.
Sisi Medeama tunaenda kufuzu kundi hili na nichukue nafasi hii kuwashukuru watu wa Kumasi, na bado nawaomba watuunge mkono Ijumaa hii na hatutawaangusha.
Rais wa Medeama SC, Moses Armah
Yanga na Medeama zitakutana siku ya Ijumaa ikiwa kila timu imecheza michezo miwili kwenye kundi D, Yanga ikiwa na alama moja ikipoteza mchezo mmoja na kutoa sare mchezo mmoja huku Medeama ikipoteza mchezo mmoja na kupata ushindi mchezo mmoja.