Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda hii leo ameikabidhi klabu ya Biashara United kupitia kwa Rais wake Revocatus Rugumila kiasi cha Million 5 ikiwa ni sehemu ya ahadi aliyoitoa kwa klabu.
Mtanda aliahidi kuipatia Biashara United kiasi hicho cha pesa baada ya kupata alama sita [6] katika michezo miwili ya Championship kati ya Cosmopolitan na Green Worriors.
Biashara United ilipata alama tatu katika mchezo wao dhidi ya Green Worriors na mchezo dhidi ya Cosmopolitan utapigwa leo katika dimba la Uhuru, jijini Dar Es Salaam huku Mtanda akiwa na imani timu hiyo itaondoka na alama tatu [3] katika mchezo huo.
Pesa hizo tayari wamekabidhiwa wachezaji na benchi la ufundi la klabu hiyo na hivyo leo wana deni la kumlipa mkuu wa Mkoa Said Mtanda.
Biashara United imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono michezo nchini.
Tunaendelea kujivunia uwepo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono michezo nchini hususani soka.
Mwenyezi Mungu awape Afya njema Rais na mkuu wa Mkoa wetu, Viongozu wa klabu, wachezaji na mashabiki wote wa Biashara United Mara.
Rais wa Klabu ya Biashara United.
Mkuu wa mkoa wa Mara siku zote amekuwa anahitaji kuona mkoa wa Mara unapata timu itakayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara na ndio maana amekuwa akiweka nguvu katika kutoa motisha kwa klabu ya Biashara United.